Marekani yamaliza mchakato wa kuiondoa Sudan kwenye orodha ya Ugaidi






Marekani imetamatisha mchakato wa kuiondoa Sudan kwenye orodha yake ya nchi zinazofadhili ugaidi.
Idara ya hazina nchini Marekani imesema: ''ofisi ya udhibiti wa mali za nje (OFAC) inafanyia marekebisho orodha hiyo kuondoa Sudan kama Mdhamini wa Ugaidi."

Uamuzi huo umefikiwa rasmi na ulianza kufanyiwa kazi Jumatatu.

Tarehe 14 mwezi Desemba, Marekani iliiondoa Sudan kwenye orodha, na kuhitimisha miaka 27 ya vikwazo vya Marekani na athari za kiuchumi nchini humo. Ulikuwa ushindi mkubwa kwa Waziri Mkuu wa serikali ya kiraia Abdalla Hamdok na serikali yake.

Nchi hiyo iliwekwa kwenye orodha ya Marekani baada ya shambulio la kwanza kwenye Kituo cha Biashara Ulimwenguni huko New York mnamo 1993, wakati Sudan ilipokuwa na vikundi kadhaa vya wapiganaji wa Kiislamu na vile vile kiongozi wa al-Qaeda Osama bin Laden.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad