Mbunge Alia na Wingi wa Wanafunzi





Mbunge wa Temeke (CCM), Dorothy Kilave ameihoji Serikali ina mpango gani wa kujenga shule katika jimbo la Temeke kwa sababu wana watoto wengi wa darasa la kwanza akidai wanatokana na wananchi wa eneo hilo kuzaliana sana.

 

“Tutakapofika mbali naamini shule za sekondari hazitaweza kutosha Vituka, Tandika. Naibu Waziri utakapokwenda na mbunge wa Mbagala upo tayari kwenda na Temeke,” amehoji Dorothy katika swali lake la nyongeza leo Jumatano Mei 5, 2021 bungeni mjini Dodoma.

 

Akijibu swali hilo naibu Waziri wa Tamisemi, David Silinde amesema yuko tayari kwenda na mbunge huyo katika jimbo hilo, “tutakwenda wote na wewe katika maeneo ya Vituka, Tandika tunafanya kazi ya wananchi na ninyi wote mnafahamu Serikali ya awamu ya sita imedhamiria kuondoa tatizo la madarasa nchi nzima.

 

”Katika swali la nyongeza la mbunge wa Mbagala (CCM), Jafari Chaurembo amesema sera ya Serikali ni kuwa na sekondari kila kata na kuhoji ni lini itapeleka shule katika kata za Mbagala na Kilungule.

 

Akijibu swali hilo, Silinde amesema mpango wa Serikali ni kujenga shule za sekondari katika kata ambazo hazina sekondari.

 

Amesema katika mwaka wa fedha 2021/22 Serikali imepanga kujenga shule za sekondari 1,000 ikiwemo na kata hizo ambazo hazina shule za sekondari katika jimbo la Temeke.

 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad