Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage amesema Wananchi wanamwona kama mchawi kutokana na Wanafunzi kufariki wakisafiri kwenye Mitumbwi wakati wa kwenda Shuleni kwasababu yeye ndiye aliyehamasisha Watoto kupelekwa Shule
Ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Elimu na TAMISEMI kupeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa Mabweni katika Shule ya Bumbile ili Wanafunzi waache kusafiri kila mara kwenda Shuleni
Ameongeza kuwa yeye pamoja na Wataalamu walinusurika kifo mwezi Februari kwasababu kutulia au kuvurugika kwa Ziwa hakutabiriki na hali huweza kubadilika wakati wowote tu