Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba SC na Yanga SC iliyokuwa ianze saa 11 jioni sasa itaanza saa 1 usiku.
TFF imesema imepokea maelekezo ya mabadiliko ya muda wa kuanza mchezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Tayari timu husika zimeshapewa taarifa ya mabadiliko hayo kupitia Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB).