Mtangazaji Casto Dickson ametangaza rasmi kuacha kazi katika kituo cha Clouds Media. Mtangazaji huyo aliyekuwa anafanya kipindi cha Siz kitaa, amewahi kutajwa kuwa moja kati ya watangazaji bora wa vipindi vya burudani nchini.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Casto ama Mwananchi kama ambavyo anapenda kujiita, ame-share taaarifa hiyo ya kuacha kazi sambamba na kuomba kuanzia sasa biashara yoyote inayojihusisha na jina lake ipuuzwe.
Pia awataka mashabiki wake wamuunge mkono atakapoelekea.