Mtoto Aliyefanyiwa Upasuaji wa Uti wa Mgongo Kabla Hajazaliwa




“Kuna hatari zake lakini upasuaji huu utamaanisha kuwa nimejitahidi katika kila namna kumchagulia kilicho bora kwake. Kwangu, ninachojua ni kwamba hakukuwa na chaguo jingine sikuwa na namna nyengine.”

 

Baada ya kujaribu mara sita bila mafanikio, kuhifadhi mayai na kutungisha mimba nje ya tumbo la uzazi, Helena alikuwa amekata tamaa kabisa ya kupata mtoto wa pili. Lakini alipojaribu kwa mara ya saba akafanikiwa kupata ujauzio na mambo yakaonekana kwenda sawa hadi mimba yake ilipotimiza wiki 20.

 

Helena akaarifiwa kuwa mtoto wake amepinda uti wa mgongo.

“Alikuwa na jeraha nyuma ya mgongo wake na nusu ya mgongo ulikuwa umeathirika. Madaktari wakamuarifu kuwa kuna uwezakano mkubwa mtoto wake akapooza, na kwamba baadaye atahitajika kuwekwa bomba la kukausha majimaji kutoka kwenye ubongo wake,” Helena anakumbuka.

 

“Wakati wananielezea kinachoweza kutokea katika hali hii, sikuwa na cha kufanya zaidi ya kububujikwa na machozi tu. Walinielezea uwezekano wa yeye kutembea au kuweza kusongeza miguu yake ulikuwa wa chini mno na hilo lilikuwa linakatisha tamaa.”

 

Thamani ya maisha

Ndani ya siku kadhaa, Helena alikuwa ameelekezwa kwenda kufanya vipimo kadhaa na kufahamishwa kuwa anaweza kufanyiwa upasuaji kabla mtoto hajazaliwa. Akiwa na ujauzito wa wiki 23, alikwenda kumuona daktari aliyebobea huko Ubelgiji katika hospitali iliyokuwa na ushirikiano na hospitali ya taifa.

 

Timu ya madaktari 25 walifanya upasuaji usio wa kawaida kurekebisha uti wa mgongo wa mtoto wake na kuziba shimo lililokuwepo mgogoni. “Nilijua ikiwa nitakosa kufanyiwa upasuaji ule maisha ya mtoto wangu hayangekuwa kama ya watoto wengine,” Helena amesema.



Profesa Anna David, daktari bingwa wa watoto chuo kikuu kimoja cha London, amesema: “Awali, tulikuwa tumeamua kuwa mtoto afanyiwe opasuaji huo baada ya kuzaliwa lakini kwasababu upasuaji huo unaweza kufanyika akiwa bado yungali tumboni, tatizo litatatulia mapema zaidi na kumaanisha kwamba athari ya uti wa mgongo itapungua zaidi.

 

“Hilo linaongeza uwezekano wa mtoto kutembea na kuthibiti kibofu chake cha mkojo na matumbo yake.” Helena akajifungua msichana wake Mila lakini baada ya miezi mitatu tangu upasuaji ulipofanywa, Mila bado anaonesha kuwa na maji maji katika ubongo wake, lakini ameonesha dalili za hali yake kuimarika.

 

‘Anatoa Shukrani Zake’

“Miguu yake sasa naweza kusonga” amesema Helena, ” ameanza kupata hisia upande wa miguuni. “Nashukuru sana madaktari waliofanya upasuaji huo kwasababu maisha yake yangekuwa tofauti kabisa kama upasuaji haungefanyika.”

 

Kupinda kwa uti wa mgongo, ambako kunaathiri takriba mimba 1,500 kwa mwaka kote nchini Uingereza, ni tatizo ambalo linazuia uti wa mgongo kukua kama inavyostahili. Na tatizo hilo linaweza kusababisha kupooza, matatizo ya tumbo na figo.

 

Lakini madaktari wakiweza kufanya upasuaji mwanamke akiwa na ujauzito kati ya wiki 22 na 26 badala ya kusubiri hadi mtoto atakapozaliwa, hutoa fursa kubwa kwa tatizo hilo kurekebishika na mtoto kukua akiwa sawa. Huko Uingereza, watoto 32 wamefanyiwa upasuaji huo tangu Januari 2020.

 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad