Mtu aliyehusika na utekaji nyara wa mamia ya wanafunzi wa kiume ameripotiwa kuuawa kwa kupigwa risasi katika jimbo la Katına nchini Nigeria.
Mapigano yalizuka kati ya magenge mawili yenye silaha katika msitu wa Dumburum ulioko katikati ya majimbo ya Katsina na Zamfara
Katika mapigano hayo, Auwal Daudawa ambaye alihusika na utekaji nyara wa mamia ya wanafunzi wa kiume mnamo Desemba 11 katika wilaya ya Kankara jimbo la Katsina, alipigwa risasi na kuuawa.
Wanachama wa genge lenye silaha walishambulia shule ya bweni wilaya ya Kankara, na kuwateka nyara zaidi ya wanafunzi 500.
Wakati wanafunzi 287 waliokolewa kufuatia shambulizi lililoandaliwa na kundi lenye silaha usiku huo, wanafunzi wengine waliachiliwa kwa makubaliano kati ya serikali na kundi lenye silaha mnamo Desemba 18.
Gavana wa Katsina Aminu Bello Masari alikuwa ameamuru shule zote za bweni katika jimbo zifungwe baada ya shambulizi hilo.