Museveni: Mafuta yasitufanye tukabweteka






Rais wa Uganda, Yoweri Museven amewaasa Watanzania na Waganda kutobweteka na mradi wa bomba la mafuta ghafi unaotekelezwa katika nchi hiyo na Tanzania, akitaka fedha zitakazopatikana kutumika kuimarisha sekta nyingine.
Kiongozi huyo mkuu wa nchi ya Uganda ameeleza hayo leo Alhamisi Mei 20, 2021 wakati wa utiaji saini utekelezaji wa ujenzi wa bomba hilo kutoka Hoima-Uganda hadi rasi ya Chongoleani, mkoani Tanga nchini Tanzania.

“Ninapenda kuwasihi wananchi wa Uganda na Tanzania wasibweteke na kulewa na mafuta na gesi wakasahau sekta nyingine kama vile kilimo cha kibiashara na viwanda  zitasaidiwa, fedha za mafuta huwa zina ukomo wake lakini kilimo kinaendelea hakina ukomo.”

“Pia utalii ili mradi mazingira yametunzwa kwa hiyo tutatumia rasilimali hizi zenye ukomo ili kuendeleza rasilimali endelevu,” amesema Rais Museveni.

Amesema ni muda wa kutumia fedha hizo kuwezesha vitu vingine ili wakati mafuta yanafikia ukomo wake nchi ziwe katika hatua nyingine ya maendeleo.

Rais Museveni amesema Uganda inahitaji gesi kwa ajili ya viwanda vya chuma, kutoa oksijeni katika matabaka ya vyuma na matumizi mengine.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad