Mzee Yusuph afunguka chanzo cha kukamatwa na Polisi Chanzo





Weekend iliyopita ilisambaa picha mitandaoni ikimuonesha mkali wa Taarab Mzee Yussuf amekamatwa na polisi akiwa amefungwa pingu, sasa Mzee Yussuf amesema sababu za kukamatwa ni wafanyakazi wake kuanzisha vurugu.
 Mzee Yussuf amesema alishtakiwa na mgonjwa wa akili ambaye anadai alipigwa na wafanyakazi wake mbele ya ofisi yake.

"Nilikuwa na kesi ya kawaida tu, kuna jamaa alinishtaki ambaye ni mgonjwa wa akili anadai alipigwa na wafanyakazi wangu mbele ya ofisi zangu, hivyo nikaitwa kama Meneja kufuatilia hilo jambo nikachelewa kwenda maana nimeitwa kama mara tano halafu sijaenda, hivyo wakaleta Askari wakanifuata" amesema Mzee Yussuf

Mzee Yussuf ameongeza kusema kwamba kesi sio yake ila alitajwa kama anahusika kwa hiyo alitoa maelezo zaidi kituo cha polisi na kinachoendelea kwa sasa ni kuripoti kituoni kwa siku alizopangiwa ili kuweka sawa mambo yaishe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad