Rais Biden azungumzia ukuta wa mpaka wa Mexico




 Rais wa Marekani (USA) Joe Biden, alitangaza kwamba wamedhibiti ufurikaji wa wahamiaji kwenye mpaka wa Mexico na kupunguza harakati za uvukaji kwa kiasi kikubwa.
Katika mahojiano yake na NBC, Biden alifanya tathmini juu ya ufurikaji wa wahamiaji katika mpaka wa kusini mwa nchi na shida ya watoto kwa kusema,

"Sasa idadi inapungua kwa kiasi fulani, tuna udhibiti kamili."

Biden alishutumu utawala wa Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump baada ya kukumbushwa kwamba "wahamiaji elfu 170 walivuka nchi hiyo mnamo Aprili, hii ni rekodi ya miaka 20 na kwamba watoto elfu 22 sasa wako Marekani."

Akiashiria kwamba kuna ufurikaji wa wahamiaji nchini kila Aprili, Biden alisema kuwa serikali ya Trump haikuwa na mpango wa suala hili.

Akisisitiza kuwa kuna mabadiliko makubwa katika mfumo wa uhamiaji kwa sasa, Biden alitoa wito kwa familia za Mexico na nchi za Amerika ya Kati kutopeleka watoto wao  Marekani wakiwa peke yao.

Biden alisema, "Wanajiweka hatarini kwa kutembea maelfu ya maili. Unaweza kuomba uhamiaji kutoka nchi yako bila kuhitaji safari hii."

Wakati huo huo, afisa mmoja kutoka utawala wa Biden alisema kuwa fedha kutoka kwa bajeti ya ulinzi kwa ajili ya miradi ya ukuta wa mpaka wa Mexico ambayo ilianzishwa chini ya Rais wa zamani Donald Trump imefutwa, na fedha zingine zitatumika kuzuia uharibifu wa mazingira unaosababishwa na ukuta.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad