Rais Joe Biden kujiunga na mkutano wa Bucharest-9





Rais wa Marekani Joe Biden atajiunga kwa njia ya vidio na mkutano wa Jumuiya ya kujihami ya NATO wa nchi za Ulaya Mashariki, unaofanyika leo Jumatatu katika mji mkuu wa Romania, Bucharest. 
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi za marais wa Romania na Poland. Mkutano huo wa viongozi unawakilisha kile kinachofahamika kama Bucharest-9, ambalo ni kundi la nchi wanachama wa NATO kutoka upande wa Mashariki. 

Nato kimsingi ni Jumuiya ya muungano wa kijeshi ya Magharibi. Nchi hizo za Mashariki wanachama wa Jumuiya hiyo, nyingi zina wasiwasi mmoja kuhusu juhudi za Urusi za kutaka kupenyeza ushawishi wake katika ukanda wao. 

Rais Klaus Lohannis wa Romania ambaye ni mwenyeji wa mkutano huo amesema kupitia ujumbe wake wa Twitta kwamba anafuraha ya kumkaribisha rais Biden na kwamba mkutano huo ni wa maandalizi wa mkutano kamili wa kilele wa jumuiya hiyo utakaofanyika mwezi ujao.

Bucharest 9 ni kundi linalozijumuisha Romania,Poland,Hungary,Bulgaria,Jamhuri ya Czech,Slovakia,Estonia,Latvia na Lithuania.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad