Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amemteua Martha Koome kuwa Jaji Mkuu wa nchini humo.
Kabla ya uteuzi huo, Bunge la Kenya lilimuidhinisha mwanamama huo.
Baada ya kuapishwa Bi. Koome atakuwa mwanamke wa kwanza nchini Kenya kushikilia wadhifa huo .
Wabunge siku ya jumatano walipiga kura kupitisha ripoti ya kamati ya bunge kuhusu haki na masuala ya sheria ambayo iliidhinisha pia kuteuliwa kwake ili kuichukua nafasi ya jaji mkuu mstaafu David Maraga