RAIS wa Sudan Kusini Salva Kiir amelivunja bunge, hatua inayotoa njia ya uteuzi wa wabunge kutoka pande kinzani katika nchi iliyokumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka mitano.
Wanaharakati na mashirika ya kijamii wanasema hatua hiyo ilipaswa kufanywa muda mrefu uliopita
Mkataba wa amani uliosainiwa miaka mitatu iliyopita uliamua kwamba karibu robo ya wabunge watatoka kwa chama cha hasimu wa zamani wa Bw Kiir, Riek Machar.
Wengi wa wabunge 550 watatoka kwa chama kinachotawala cha SPLM,wabunge wa Sudan Kusini hawatachaguliwa lakini badala yake watateuliwa na vyama tofauti vya kisiasa.