Rais Samia awapangua Ma RC Kafululi, Mongella




 

Rais Samia Suluhu Hassan
RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko madogo ya wakuu wa mikoa, kwa kumpeleka John Mongella Arusha na David Kafulila Simiyu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ni baada ya kumaliza kuwaapisha, leo Jumatano, tarehe 19 Mei 2021, Ikulu ya Dar es Salaam.

Awali, Rais Samia alimteua Mongella kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kutoka Mwanza na Kafulila Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Amesema, amefanya mabadiliko hayo kwa kuwa, Kafulila ni mgeni katika nafasi hiyo huku Mongella akiwa na uzoefu wa kuongoza mkoa mkubwa.


 
Awali, Kafulila alikuwa Katibu Tawala (RAS) mkoani Songwe na Mongella alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.


“Nimefanya mabadiliko kwa wakuu wa mikoa wawili, Kafulila ambaye alikuwa Arusha na Mongella ambaye alikuwa Simiyu, sasa nimeamua Mongella sababu ulikuwa unaongzoa mkoa mkubwa na ulikuwa unaendelea kuwa jiji na Arusha ni jiji, utakwenda Arusha,” amesema Rais Samia

“Na Kafulila sababu ndiyo anaanza alikuwua RAS na sasa mkuu wa mkoa wewe utakwenda Simiyu. Nimefanya mabadiliko hayo, maelekezo mengi mtapewa kwenye kikao cha ndani.”


Rais Samia alifanya mabadiliko na uteuzi wa wakuu wa mikoa Jumamosi tarehe 15 Mei 2021, ambapo aliteua wakuu wa mkoa wapya 10 na kuwabadilisha 16.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad