Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amewataka watumishi wa serikali na sekta binafsi kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa uaminifu ikiwemo kutojihusisha na vitendo vya rushwa pamoja na ubadhirifu wa mali.
Kauli hiyo ameitoa hii leo Mei 14, 2021, Jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu pamoja na viongozi wa dini mbalimbali waliohudhuria Baraza la Eid lililofanyika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.
"Niwasihi watumishi wa serikali na sekta binafsi wahakikishe wanafanya kazi na kupata kipato cha halali, wajiepusha na vitendo vya wizi, rushwa, ubadhirifu na urasimu na wafanyabishara walipe kodi stahiki kwa serikali," amesema Rais Samia