Sakata la Gigy Money kufungiwa laibuka kikao cha wasanii na Bashungwa





Sakata la msanii wa Bongofleva, Gift Stanford maarufu Gigy Money kufungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kujihusisha na sanaa ndani na nje ya nchi kwa miezi sita limeibuka katika kikao cha wadau wa sanaa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa.
Kikao hicho kinafanyika leo Jumamosi Mei 8, 2021 mkoani Dar es Salaam kujadili masuala mbalimbali likiwemo la nyimbo za wasanii kutochezwa mahali popote mpaka zihakikiwe na Basata.

Gigy alifungiwa Januari 5, 2021 akidaiwa kuwa katika tamasha la Wasafi ‘Tumewasha Tour’, lililofanyika jijini Dodoma, msanii huyo alipanda jukwaani kwa ajili ya kutumbuiza na kuvua gauni (dela) na kubaki na vazi lililoonyesha maungo yake ya mwili.

Leo wakati kikao kikiendelea msanii Wakazi aligusia kufungiwa kwa Gigy akibainisha kuwa vazi alilokuwa amelivaa ni la ubunifu lakini ikatafsiriwa kuwa ni kosa la kimaadili.

"Tunaomba waziri kama itakupendeza Gigy Money angefunguliwa kwani ni mama mwenye mtoto na anategemea kazi hii kujipatika riziki,” amesema Wakazi

Wakati akiendelea kuzungumza Bashungwa alimkatiza, na kumtaka kuachana na mambo ya Gigy kwa kuwa si ajenda ya kikao hicho, akitaka utafutwe muda mwingine.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad