Nimekuwa nikizifuatilia sana Tweet za MO Dewji ambaye ni Kiongozi wa Simba, nikiri wazi kuna Tweets zingine ni contraversial sana, hutarajii zitoke kwake
Tweet hii ya leo kusema wamewaoutplay Kaizer na wamewafanya kuwa Mediocre! Inafikirisha sana, inafikirisha kwenye engo nyingi
Mosi, nani Mediocre kati ya yule aliyeko nje ya michuano na yule anaesonga mbele, Simba wapo nje na Kaizer wapo nusu, who is the mediocre hapo
Pili, anasema wamewaoutplay Kaizer lakini yeye aliitumia FNB vizuri akampa Simba 4-0, nae Simba katumia vizuri Mkapa ila sio kama alivyotumia Kaizer, sasa nani kawa outplayed?
Tatu, ina maana MO hajui kuwa hii sio hatua ya makundi bali hii ni hatua ya mtoano, watu wanacheza na aggregate jumlisha na hesabu sahihi kusonga mbele, hajui hilo? Watu wanacheza kwa plan zaidi
Point yangu ni ipi?
Point yangu ni MO Dewji kuacha kutengeneza Tweets ambazo hazipaswi kutoka kwa Influential figure kama yeye, nadhani anaweza kutweet kitu bora zaidi ya hivyo
Ndani ya misimu mitatu Simba kaishia robo fainali mara mbili, maana yake hiyo ndio level yake kwasasa muhimu ni wao kuja na plans kuelekea next season sio kuuficha ubora halisi wa Amakhosi
Point yangu ni kuwa as the Chairman ni muhimu zaidi kupunguza munkari kwenye mitandao yake, ajitahidi kuweka vitu muhimu kama ambavyo wenzake klabu kubwa wafanyavyo, being cool ni bora zaidi
Lakini sometimes hizi accounts za watu mashughuli wanaweza kuwa wanaendesha Maadmn kwa niaba ya muhusika, basi kama ni hivyo wajitahidi kupost vitu smart ambavyo vinaleta maana kwa watu
Ni busara kama kuna Admin anafanya hiyo kazi basi ajitahidi kulitazama hilo, hiyo post siyo relevant kwa Mtu kama MO.