Shaka aanza kupokea kero za Wananchi kupitia simu yake ili zipatiwe ufumbuzi




KATIBU  wa Itikadi na Uenezi, wa Chama cha Mapinduzi CCM , Shaka Hamdu Shaka, amesema kupitia agizo la Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo la kumtaka atoe namba ya simu yake kwa wananchi kwa ajili ya kupokea kero na changamoto mbalimbali za wananchi tayari amepokea kero  hizo za wananchi kwa njia mbalimbali za mtandao.

Amesema kwa takribani muda wa siku moja na masaa kadhaa amepokea ujumbe mfupi kwa njia ya kawaida jumbe 2974 za kero  na changamoto  na ujumbe wa njia ya WhatsApp amepokea  jumbe 2664.

Akizungumza  mkoani Dar es Salaam wakati wa mapokezi ya kumpokea Katibu Mkuu wa Chama hicho Taifa, Daniel Chongolo na Sekretarieti yake ya Halmashauri kuu, amesema  jumbe hizo alizopokea  zilizokuwa na  viambatanisho na vielelezo vya kero mbalimbali za wananchi. 

Shaka  amesema hiyo inaashiria kwamba  Sekretarieti  hiyo na Chama chao wanayokazi yakufanya hivyo amehaidi kuanza kuzishughulikia huku akiwataka watendaji wa chama na serikali kuzifanyia kazi changamoto hizo, kila mmoja kwa nafasi yake  atimize wajibu wake kwa nafasi yake.

"Nataka niwahakikishie watanzania kuwa Sekretarieti hii imebeb maono na imebeba mtazamo ipo tayari kutekeleza kwa vitendo adhima  na nia ya Rais Samia Suluhu Hassan,"amesema na kuongeza,

"Tunakwenda kusimamia kero,changamoto, haki na dhuruma kuwahakilishia watanzania wanafikia mwisho wake kwani Rais Samia Suluhu Hassan aliwahi kusema Uongozi ni kuonyesha nia na sio kufunga njia,"amesema.

Amewataka viongozi wa Serikali walioteuliwa kufanya kazi kwa bidii kwani, wakati huu wanapaswa kujituma kuhakikisha kazi inaendelea.

 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad