Simba kukwea pipa kuifuata Kaizer Chiefs kesho






Kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes raia wa Ufaransa kesho Mei 11 kinatarajia kukwea pipa kuelekea nchini Afrika Kusini.

Simba ni wawakilishi wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo kwa sasa wametinga hatua ya robo fainali baada ya kuwa vinara wa kundi A wakiwa na pointi 13.

Mei 15 itakuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya Kaizer Chiefs kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni robo fainali ya kwanza.

Kwa mujibu wa Kocha Mkuu, Gomes amesema kuwa wanatarajia kuondoka leo Jumatatu kwa ajili ya kuwafuata wapinzani wao.

"Jumnne alfajiri (saa 9:45) tunatarajia kuondoka Tanzania kuelekea Afrika Kusini," .

Wachezaji wa Simba watakwea pipa wakiwa na kumbukumbu mbaya ya mchezo wao dhidi ya watani wa jadi Yanga kuyeyuka kutokana na mkanganyiko ulitokea Mei 8.

Mchezo huo ulitarajiwa kuchezwa saa 11:00 jioni ila Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) lilitoa taarifa kwamba utachezwa majira ya saa 1:00 usiku jambo ambalo liligomewa na Yanga kwa kueleza kuwa ni kinyume na kanuni.

Kwa sasa TFF wameeleza kuwa wanalifanyia kazi suala hilo ili kujua hatma ya mchezo huo ambao umesababisha hasara kubwa na inakuwa ni rekodi ya kwanza kwa miaka ya hivi karibuni kutokea.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad