Simba Haji Manara leo Mei 19, 2021 akiongea na wanahabari ameweka wazi kuwa hawahitaji kujitahidi kuelekea kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs, Mei 22, 2021 utakaochezwa Uwanja wa Mkapa. Mgeni rasmi katika mchezo huo atakuwa Mkuu wa Mkoa mpya wa Dar es Salaam, Amos Makala.
Simba watakuwa wenyeji wa Kaizer Chiefs katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao utapigwa Jumamosi hii katika Uwanja wa Mkapa, Dar.
Simba watalazimika kushinda mabao 5-0 kwa ajili ya kukata tiketi ya kuingia hatua ya nusu fainali baada ya kupoteza mchezo wa awali kwa mabao 4-0.
Simba imeweka wazi kwamba wanaweza kuwafunga mabao matano zaidi kwenye mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Ili Simba itinge hatua ya robo fainali ni lazima ishinde zaidi ya mabao matano kwa sababu ule mchezo wa kwanza walikubali kichapo cha mabao manne kwa bila.
“Kama uongozi tumejiandaa na mchezo wa Jumamosi. Tunaamini wachezaji watapokea maelekezo vizuri kutoka kwa walimu na tutashinda.”
“Kama tunahitaji kushinda Jumamosi lazima wachezaji wetu wajitoe kwa asilimia 100, wanaweza wakiamua.”
“Wanasimba wanataka kufuzu, hatutaki kujitahidi, Simba sio timu ya kujitahidi, ni timu ya kufuzu. Mashabiki wanaiamini timu yao inaweza.”
“Mpaka sasa tumeruhusiwa mashabiki 10,000 lakini tunaendelea kuomba kuongeza. Naomba uwanjani rangi iwe nyekundu na nyeupe.”- Haji Manara.