Spika awapa mbinu CHADEMA ili awafukuze akina Mdee

 


Spika wa Bunge Job Ndugai, amemuagiza Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Mnyika, kuandika barua ambayo ataambatanisha na katiba ya chama chake pamoja na muhtasari wa kikao kilichofanya maamuzi ya kuwafukuza uanachama wabunge 19 wa chama hicho.



kushoto ni Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika na kulia ni Spika wa Bunge Job Ndugai


Kauli hiyo ameitoa hii leo Mei 3, 2021, Bungeni Dodoma, hii ni baada ya uwepo wa malalamiko kutoka kwa viongozi wa chama hicho wakimtuhumu Spika Ndugai kutozingatia katiba kwa kuendelea kukaa Bungeni na wabunge wasiokuwa na sifa za ubunge.

"Aandike barua aambatanishe na katiba ya chama chake, aniambatanishie na muhtasari wa hicho kikao kilichofanya hayo maamuzi, inawezekana huyo Katibu Mkuu kaamka tu kaandika halafu na mimi nakurupuka nachukua hatua, nitakua ni Spika au kitu cha ajabu, hivyo andika ili ile barua niwape watalam waangalie, halafu namuuliza msajili wa vyama hawa wajumbe walioorodheshwa ndiyo wajumbe halisi?", amesema Spika Ndugai

"Pia naangalia kwenye muhtasari ule je hawa wabunge wanaotuhumiwa kufukuzwa walipata nafasi hata ya kujieleza na walisikilizwa?, nifukuze watu ambao hawakusikilizwa popote, yaani mbunge hujawahi kusikilizwa wanaandika tu fukuza hawa, viko vyama vimejaa mfumo dume, kundi la wanaume wamekaa wanafukuza wanawake 19 kwa mpigo hata kama barua hiyo inatoka CCM lazima nitawaambia 'stop' kwanza taratibu", ameongeza Spika Ndugai.

Novemba 25, 2020, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kiliwafukuza uanachama wabunge wake 19, akiwemo Halima Mdee, Ester Bulaya, Esther Matiko, Tunza Malapo, Salome Makamba na wengineo kwa madai ya kwamba ni wasaliti baada ya kwenda kula kiapo Bungeni cha kuwa wabunge wa viti maalum kinyume na makubaliano ya chama chao.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad