Spika Ndugai Atoa Masharti kwa Vyama vya Siasa Vinavyotaka Kufukuza Wabunge




Spika wa Bunge , Job Ndugai amevitaka vyama vya siasa vinavyotaka kufukuza wanachama wao ambao ni wabunge kufuata sheria na taratibu zote kwani lazima mchakato huo utendeke kwa haki.
Aidha, ameendelea kusisitiza kuhusu wabunge 19 waliofukuzwa uanachama Chadema, akitaka kupatiwa vielelezo kuhusu kufukuzwa kwao na kwamba huo ni msimamo wa kiti.

Wabunge hao 19 akiwemo Halima Mdee walifukuzwa Chadema Novemba mwaka 2020 baada ya kuapishwa kuwa wabunge bila ridhaa ya chama hicho lakini wameendelea kuwa wabunge jambo ambalo kwa nyakati tofauti Chadema wamelipinga huku Ndugai akidai hana vielelezo.

“Maamuzi ninayotoa hapa, ni maamuzi ambayo yatatumika nami na hata watakaofuata baada yangu… Kwa vyama vyovyote vyenye kufukuza wabunge…. wanapaswa wanapomwandikia barua spika… lazima barua hiyo iambatane na katiba yao, iambatane na muhtasari au mihtasari ya vikao vilivyohusika kuwafukuza wabunge hao,” Spika Ndugai ameeleza hayo leo  bungeni mjini Dodoma na kusistiza kuwa anaposema kitu isichukuliwe kama ni Job Ndugai ndiye amesema, bali kiti cha Spika wa Bunge.  

Pika Ndugai amesema maamuzi hayo hayawalengi wabunge wa upande mmoja tu bali kwa chama chochote cha siasa  ambacho kitakuwa na nia ya kuwatimua wabunge.

Amesema kwa kufanya hivyo inarahisisha kazi yake ya kutenda haki.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad