Trump afunguliwa mashtaka ya uhalifu




Mwanasheria mkuu wa New York huko Marekani Letitia James ameifungulia mashtaka ya uhalifu kampuni ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump na kuongeza changamoto za kisheria kwa familia ya mwanasiasa huyo mwenye ushawishi mkubwa katika chama cha Republican. 
James amekuwa akichunguza iwapo kampuni ya Trump ilitoa thamani za uongo za mali zake ili ipate mikopo na kulipa kodi ya chini. Tangazo hili linaonyesha matatizo ya kisheria yanayomkabili Trump miezi minne baada ya kuondoka afisini. 

Hadi kufikia sasa Trump amefunguliwa jumla ya mashtaka matatu ya uhalifu. Kampuni hiyo ya Trump hadi kufikia sasa haijatoa tamko lolote kuhusiana na suala hilo lakini Trump mwenyewe amesema kwamba uchunguzi huo unaofanywa na mwanasheria huyo ambaye ni mdemokrat, umechochewa kisiasa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad