Nchi ya India imerekodi vifo vya watu 4,187 kwa siku moja hii leo Mei 8 na kufikisha idadi ya vifo vitokanavyo na corona kufikia 238,270 tangu mlipuko uingie nchini humo
Uchomaji wa miili ya waliofariki kwa ugonjwa wa CORONA India Ikifanyika
Maeneo ya kuhifadhi miili ya marehemu na yale ya kuchomea miili yamejaa kiasi cha kusababisha miili kwenda kuchomewa katika maeneo ya kuegesha magari na mbuga
India imefikisha wagonjwa wa corona wapatao milioni 21.9 huku wataalamu wa afya wakionesha wasiwasi wa kuongezeka vifo na wagonjwa kufuatia maambukizi mapya yanayotarajiwa katika mwezi huu na kushauri uchukuliwaji wa hatua za mapema.
Waziri Mkuu wa nchi hiyo Narendra Modi amelaumiwa kwa kushindwa kupatikana kwa oksijeni za matibabu, huku katika taarifa ya serikali ikisema itafanya kila linalowezekana zipatikane