Ikiwa leo ni siku ya Africa, msanii wa HipHop hapa nchini Webiro Wasira 'Wakazi' amesema haoni noma watu kuiga na kujifunza utamaduni mwingine wa nje ya bara la Africa haswa kwenye kazi za sanaa.
"Hakuna ubaya wowote kwenye kuiga Tamaduni zingine kwa kuzifuatilia tamaduni na sanaa za nje ya bara la Africa, Dunia ishakuwa kijiji na teknolojia inatuwezesha kupata vitu vya kila sehemu na tukajifunza, Tamaduni pia zinabadilika kutokana na muda na mahali"
"Hata ukiingalia Afrika yenyewe kuna vitu vingi ambavyo tunaviita Mila, Tamaduni tuliviiga na kuvijifunza kutoka kwa Waarabu, Wareno na Waingereza kipindi cha Ukoloni, hakuna shida ni sawa mtu kufuatilia vitu vya sehemu nyingine na kupata tamaduni za nje ya Africa" ameeleza Wakazi
Wakazi ni mmoja wa wasanii walioshiriki kikao cha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Innocent Bashungwa juu ya kupanga utaratibu mpya kwa wasanii na kazi zao za sanaa.