Wakazi wa Gaza washindwa kupata usingizi Kisa Mabomu



Mashambulizi ya anga na maroketi yalioendelea kuvurumishwa katika mzozo Israel na Gaza yamegharimu maisha ya watu zaidi huku miito ya kusitishwa mapigano hayo kutoka pande tofauti za ulimwengu ikiendelea kutolewa.

Weltspiegel 18.05.2021 | Israel - Palästina

Mwandishi wa habari wa Shirika la Habari la Ufaransa AFP amesema kumesikika mashambulio ya mara kwa mara katika mji wa Gaza, huku baadhi ya wakazi wa mji huo wakishindwa kupata usingizi kutokana na wasiwasi wakati ndege za kivita za Israel zikipita angani.

Na mjini New York mkutano wa Baraza la Usalama wa Umoja wa Mataifa ulisitishwa pasipo kutoa taarifa yoyote kuhusu hali hiyo lakini Ufaransa ilisema imetoa azimio la kupendekeza kusitishwa mapigano, ikishirikiana na majirani wa Israel, Misri na Joradan.

Ulaya imetoa wito wa kusitishwa mapigano.

Israel - Palästina-KonfliktMwandamanaji wa Kipalestina akikabiliana na jeshi la Israel
Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wametoa wito wa kusitishwa mapigano kati ya Israel na Hamas, mkuu wa sera za nje za umoja huo wenye mataifa 27, Josep Borrel amesema Hungary imekataa kusaini taarifa ya pamoja kuhusu mzozo huo.

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel na Mfalme Abdullah wa Pili wa Jordan wametaka jitihada za kuandaa mazingira ya kuanzisha kwa mazungumzo ya usuluhishi ya kisiasa.

Lakini pamoja na miito hiyo ya kimataifa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu Jumanne alisisitiza kuendelea na mapambano hadi kufanikisha hali ya usalama kwa Waisrael. Kwa mujibu wa wizara ya afya yaGaza, mapigano hayo yanayopindukia wiki moja, yamesababisha kuuwawa kwa Wapalestina 217, wakiwemo watoto 63, na kuwajeruhi zaidi ya watu 1,400.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad