Kikundi kimoja cha imani ya Rasta nchini Kenya kimeenda mahakamani wakitaka kuruhusiwa kutumia bangi kwa madhumuni ya 'kiroho'.
Jumuiya ya Rastafari ya Kenya, inayojitambulisha kama kikundi cha kidini kidogo, ilisema washiriki wake wanaishi kwa hofu kwa sababu ya sheria ambazo ni kikwazo kwa shughuli zao za kiroho.
Ilisema wanachama wake mara nyingi walikuwa wakinyanyaswa, kutishwa, na kupekuliwa bila sababu katika nyumba zao za binafsi au sehemu zilizotengwa.
Kikundi kilisema matumizi ya bangi yanaruhusiwa na imani yao ya Rastafari kwa madhumuni ya kiroho, dawa, mapishi na sherehe.
Mawakili Shadrack Wambui na Alexander Mwendwa walisema kuwa bangi ni "sakramenti" inayounganisha waumini na "muumba" wao.
Wiwalaumu viongozi kwa kutohakikisha kwamba haki zao za kidini zinaheshimiwa.
Mnamo mwaka wa 2019, Mahakama Kuu nchini Kenya iliamua kwamba harakati Za Rastafarian zilikuwa kikundi cha kidini kama vingine vyovyote hivyo wanapaswa kuchukuliwa kwa usawa.
Uamuzi huo ulifuatia kesi ambapo mwanaume mmoja aliishtakishule kwa kumfukuza binti yake kwa sababu alikuwa amesokota nywele. Mzazi huyo alisema binti yake alikuwa na mtindo huo wa nywele kwa sababu familia ilijiunga na imani ya Rastafarian.
OPEN IN BROWSER