Mjomba Aliyetuhumiwa Kubaka Mtoto wa Miaka 3 Ashinda Kesi





WANANCHI wa mtaa wa Mpeto kata ya Ramadhani mjini Njombe,wameiomba Serikali kuingilia kati kesi ya mtoto wa mtaa huo aliyebakwa akiwa na umri wa miaka 3 mwaka 2018 na kusababishiwa maumivu makali pamoja na kutafutiwa njia mbadala kwa ajili ya haja kubwa na ndogo huku mjomba wake aliyetuhumiwa na kesi hiyo kushinda Mahakamani.

 

Aidha wameomba serikali kuwachukulia hatua kali wanaume wabakaji na walawiti wa watoto na kuwasababishia ulemavu kufuatia wahusika waliowengi wa matukio hayo ya kikatili kushikiliwa kwa muda na kisha kuachiwa bila kufanywa chochote.

 

Hayo yamebainishwa na wananchi hao walipojitekeza katika ofisi ya mtaa huo kuchangia mtoto wa kike aliyefanyiwa kitendo cha ubakaji mwaka 2018 na kupata ulemavu ambao unagharimu fedha nyingi kwaajili ya matibabu katika hospitali ya taifa ya Mhimbili.

 

“Kwasababu wananchi tumekusanyika hapa kwa maana hiyo jambo hili linafahamika kiserikali,kwa hiyo jambo langi la kwanza nitoe rai kwa vyombo vyote vya serikali juu ya hili swala kwasababu sisi tumeonyesha njia kuwa kuna jambo huku na mtoto anahitaji msaada”alisema Alex Mwalongo mkazi wa mtaa huo.

 

Baadhi ya wananchi akiwemo Betrice Malekela mwenyekiti wa UWT wilaya ya Njombe na Erasto Ngole Katibu wa siasa na uenezi wa chama cha mapinduzi mkoa wa Njombe,wamesema kuwa vitendo vya ubakaji vinashamiri mkoani Njombe kutokana na jamii kukaa kimya pindi matukio hayo pamoja na kukkubali kuyamaliza katika ngazi ya familia.

 

“Tumeona kabisa mtoto huyu alivyofanyiwa kwanza ni mtoto mdogo kwa kweli ni kitendo cha ukatili na familia yake ni duni kwa hiyo hapa leo jamii na wanawake wamejitokeza kwa wingi na kupaza sauti ili jamii ijifunze”Alisema Betrece Malekela.

 

Naye Erasto Ngole alisema; “Kwa sisi wanaume hiyo ni aibu,mwanaume ameamua kumbaka mtoto mdogo na wanasema wakati huo akiwa na miaka 3.”

 

Wanafamilia akiwemo mama wa mtoto huyo bi,Atu Mkane pamoja na bibi yake wameeleza namna tukio hilo lilivyotokea pamoja na hatua mbalimbali walizochukua.

 

“Ilifika saa tisa usiku akaja kuniamsha bibi ake akaniambia mtoto umemchukua nikasema hamna tukatoka nje tukaona mtoto amelala nje akiwa amechanika vibaya mno ndio tukaanza kumpeleka zahanati ya Nyombo na kibena ndio matibabu yaikoanzia”alisema mama wa mtoto.

 

Zaidi ya shilingi milioni 12 za michango ya wananchi zimepatikana kupitia kampeni ya tunaishi nayo inayoendeshwa na moja ya kiuo cha radio wilayani Njombe na kukabidhiwa mama wa mtoto Hakima Kilowoko mkazi wa Mpeto mjini Njombe,kwa ajili ya matibabu yanayoghalimu zaidi ya milioni nne.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad