WATAALAM wa masuala ya utafiti Duniani wamesema wanaume ambao wana wachumba/wake wanene huishi maisha marefu na yenye furaha ikilinganishwa na wale wenye miili ‘midogo’ (wembamba).
Hii ni kulingana na utafiti uliofanywa na Dkt. Filemon Alvarado na Dkt. Edgardo Morales kutoka Idara ya Saikolojia katika taasisi ya UNAM’s ya Chuo Kikuu kimoja nchini Mexico kilichopo Mexico City.
Aidha, utafiti huo umebainisha kuwa wanawake wanene huwa wana ujasiri na mara nyingi hawakasiriki upesi. Bw. Musyoka John ambaye ana mke ‘mwembamba’ ameeleza kuwa mara nyingi mkewe humhangaisha na hawana uhusiano mzuri katika ndoa yao.
Ameeleza kuwa mkewe anapoamua kufanya jambo ama kukataa, kamwe hawezi kugeuza msimamo wake. Kulingana na utafiti huo, wanaume wanaotaka kuishi maisha marefu wanapaswa kuwaoa wanawake wanene.
Bila kujali saizi ya maumbo, wanaume wengi hupenda wanawake wembamba na wale wenye miili ya wastani lakini wachache hupenda wanawake wanene.
Mambo ambayo hata wao hawayajui ni kwamba, wanawake wembamba wanazo baadhi ya tabia ambazo zinahitajika sana katika maisha ya ndoa.
Miongoni mwake ni;
1. Kujali; Dkt. Filemón Alvarado na Dkt. Edgardo Morales wanasema wanawake wembamba wanauwezo mkubwa wa kumjali mwanamme na wanazungumza kwa upole.
2. Ukweli; Inaelezwa pia kuwa wanawake wanene ni wakweli, wako karibu zaidi na waume zao lakini ni wa gharama kubwa. Hii sio hukumu kuwa wanafaa sana kuliko wanawake wengine.
3. Utu; Asilimia kubwa ya wanawake wanene ni wanyenyekevu, wanavutia, ni wanyenyekevu na wanawathamini wenza wao.
4. Kujitegemea; Wanawake wengi wanene wanatajwa kuwa ni wapambanaji, hujituma na mara nyingi hawawategemei wanaume kuwatunza. Wanao uwezo wa kufanya kazi ama biashara kujiingizia vipato, sio ‘magolikipa’.
5. Mahaba; Tafiti hiyo inaeleza kuwa wanawake wanene wana mahaba mazito ambayo huwavutia na kuwapa raha waume zao.
Ujumbe wa Mhariri: Makala haya hayana lengo la kuwadunisha wanawake wenye ‘miili midogo’ kwa njia yoyote ila ni kueleza mambo jinsi yalivyotajwa na waliohojiwa.
Mwandishi: Eddy Nevo na Mtandao