SERIKALI imetoa mwongozo namba sita kwa wasafi ri unaotaka abiria wageni au wakazi wanaoingia nchini kutoka nchi zenye aina mpya ya virusi vya corona wakae karantini siku 14 na kwa gharama zao.
Aidha, abiria hao watatakiwa kupimwa virusi hivyo wakiwemo wanaoingia nchini kutoka katika nchi zenye maambukizi makubwa kwa gharama ya Dola 25 za Marekani kwa kila abiria.
Hayo yamebainishwa katika mwongozo huo mpya kwa wasafiri uliotolewa juzi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Abel Makubi.
Mwongozo huo ulibainisha kuwa wasafiri watakaokaa karantini kwa lazima watachagua sehemu ya kukaa kutoka katika orodha iliyotolewa na serikali huku Watanzania wanaorejea nchini wataruhusiwa kujitenge wakiwa majumbani.
“Ikiwa abiria atawasili katika uwanja wa ndege,bandari au kituo chochote kutoka nje ya nchi, watapatiwa kadi ya taarifa za afya na kupatiwa namba kisha kushauriwa kujiangalia wenyewe iwapo wataona dalili za ugonjwa,na iwapo watabaini dalili zozote watapimwa na kupatiwa matibabu na serikali kwa gharama zao.
“Alisema Makubi Alibainisha kuwa abiria waliosafiri kwa zaidi ya saa 72 watatakiwa kupimwa tena wanapowasili nchini huku wafanyakazi wa kwenye ndege wakitakiwa kuchukua tahadhari zinazostahili na kuonesha vyeti vinavyoneshwa kupimwa ugonjwa huo.
Alisema abiria wote watakapowasili nchini watawasilisha cheti kinachoonesha wamepima na kuwa hawana maambukizi ya virusi hivyo na kuwa wamepimwa ndani ya saa 72 kabla ya kuwasili nchini.
Alisema mikakati ya nyongeza kwa madereva wa magari na malori yanayobeba bidhaa na kutoa huduma mbalimbali kuwa wanatakiwa kuwa watui wawili hadi watatu katika kila gari na katika safari zao wanaruhusiwa kudsimama katika vituo vilivyoainishwa na serikali.
Alisema ikiwa mmoja wa watu katika magari hayo atawekwa karantini akiwa safarini ,mmiliki wa magari hayo kuhakikisha hatua kumhudumia mfanyakazi wake na pia gari hilo na kuhakikisha bidhaa zinafika katika maeneo yaliyotarajiwa.