Watu 15 Wafariki Kwenye Mlipuko wa Volkano




TAKRIBANI watu 15 wamethibitishwa kufariki kutokana mlipuko wa volkano uliotokea katika Mlima wa Nyiragongo, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) lakini huenda idadi ya vifo ikaongezeka wakati maafisa wakiyafikia maeneo yaliyoathirika zaidi.



Volkano ililipuka katika mlima Nyiragongo una kumwaga ujiuji wa moto ama lava uliolifanya anga kuwa jekundu Jumamosi, lakini lava hiyo haikuhfika katika mji wa Goma unaokaliwa na watu milioni mbili kusini mwa mlima huo.



Wakazi wa vijiji vya karibu na mlima huo pamoja na mji Goma ambao waliyakimbia makaazi yao kwa hofu ya mlipuko huo wameanza kurejea huku wengi wao wakiwasaka jamaa zao waliopotea.



Watu tisa miongoni mwa waliothibitishwa kufa, walipoteza maisha katika ajali za barabarani wakati watu walipokuwa wakihaha kukimbia ili kuokoa maisha yao.



Wanne walikufa walipokuwa wakijaribu kutoroka gerezani huku wawili wakiungua hadi kufa, alisema msemaji wa serikali Patrick Muyaya Jumapili.

 

 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad