Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu atangaza kupokea msaada wa kimataifa haswa kutoka Marekani




Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alitangaza kuwa msaada wa kimataifa, haswa kutoka Marekani (USA), ulikuwa nyuma yao katika mashambulizi kwenye Ukanda wa Gaza, na kwamba mashambulizi ya Gaza yataendelea.
Katika taarifa iliyotolewa kupitia akaunti ya Twitter ya Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel, ilielezwa kuwa Netanyahu alikutana na maafisa wa ulinzi, ujasusi na wanajeshi kujadili mashambulizi ya Israel huko Gaza.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari baada ya mkutano huo, Netanyahu alisema kuwa operesheni dhidi ya Gaza itaendelea kwa nguvu kamili na akaelezea kuwa Israel inahitaji muda kufikia malengo yake na operesheni za kijeshi.

Akibainisha kuwa operesheni hiyo itachukua muda, Netanyahu alisema,

"Kuna msaada mkubwa, haswa kutoka Marekani. Kuna msaada wa kimataifa, na tunautumia."

Netanyahu pia alibaini kuwa ngome elfu moja za Hamas zililengwa huko Gaza na uharibifu mkubwa ulisababishwa, ingawa bado hazijaondolewa kikamilifu.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad