WHO yatangaza kuwa janga la Covid-19 litakuwa hatari zaidi mwaka huu kuliko mwaka jana





Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limesema kwamba mwaka wa 2021 utakuwa "mbaya zaidi" kwa sababu ya janga la corona (Covid-19), lililoibuka China mwishoni mwa mwaka 2019 na likageuka kuwa janga kubwa kwa kuenea kote ulimwenguni mnamo 2020.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema,

"Tunaamini mwaka wa pili wa janga hili utakuwa mbaya zaidi kuliko ule wa kwanza."

Akibainisha kwamba wimbi la pili la janga hilo nchini India "limeleta wasiwasi mkubwa", Ghebreyesus alisema kuwa "visa vipya vya kutisha, kulazwa hospitalini na vifo" vilirekodiwa katika majimbo mengi ya India.

Ghebreyesus alisema kuwa kama WHO, walituma bomba la oksijeni India, mahema, barakoa na vifaa vya matibabu kwa hospitali za mikoani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad