Kufuatia yaleyanayoendelea kwasasa juu ya utaratibu mpya ulioanzishwa na Baraza la Sanaa la Taifa la wasanii wote kuzipitia kazi zao kabla ya kuzipeleka kwenye vituo vya redio na tv na pia kufungiwa ngoma zao, msanii #Zanto ameoneshwa kutoridhishwa kabisa na utaratibu huo mpya
#Zanto amepinga vikali utaratibu huo huku sababu aliyoieleza ikiwa ni wapi watakapozipatia fedha hizo za kwenda kufanyia marekebisho ngoma zao, pia msanii huyu ameenda mbali za kwa kuulaani utaratibu huu mpya kwa kuandika kuwa muziki ni sehemu ya ajira hivyo wanaua mitaji yao
Star huyu amethibitisha tarifa hii kwenye ukurasa wake wa instagram kwa kuchapisha ujumbe uliosomeka ....
'@Basata.tanzania #cosota MNAUA MITAJI YA WASANII:
#muzikiniajira
Unakagua wimbo ambao tayari umeshamalizika kutengenezwa kisha mnaukataa au mnamwambia msanii akafanye marekebisho wakati kurudi studio kwenda kurekebisha yampasa msanii kulipa pesa kununua muda kwa producer ili kuirekebisha upya, hakuna misingi yyte mliyotuwekea ya kutuwezesha kupata pesa zetu zinazopotea, majina yetu, thamani yetu, bongo fleva yetu tumetengeneza kwa nguvu zetu wenyewe leo mnakuja kuua focus yetu ya kufikiria tunawekaje ushindani na kina #Wizkid #Davido badala yake tunawafikiria nyinyi mtapenda mashairi yetu au laaaa. Vipi kuhusu mirabaha? MUZIKI NI AJIRA #muzikiniajira #muzikiniajira #muzikiniajira @@samia_suluhu_hassan @innocentbash" ✍️... @z_antoofficial