Mwanaume mmoja ameruka kutoka kwenye ndege iliyokuwa inaruka katika uwanja wa kimataifa wa Los Angeles baada ya kujaribu kufika sehemu ya marubani.
Mwanaume huyo ambaye hakufahamika , alifungua dirisha la ndege na kuruka kupitia mlango wa dharura siku ya Ijumaa, mamlaka ya anga ilisema.
Alikamatwa na kupelekwa hospitalini akiwa na majeraha. Kumekuwa na ongezeko la matukio ya ndege nchini Marekani.
Matukio yapatayo 3,000 yamerikodiwa mwaka huu. Tukio la Ijumaa lilitokea majira ya saa moja na dakika 10 katika saa za Marekani katika ndege ya United Express flight, inayomilikiwa na SkyWest Airlines.
Wafanyakazi wa ndege waliripoti kumuona abiria huyo akinyanyuka kwenye kiti chake kwenye ndege na kuanza kuanza hekaheka za kutoka.
Walisema aligonga mlango wa chumba cha marubani kabla hajaondoka kwa kupitia mlango wa dharura, NBC News imeripoti.
Ndege hiyo baadae iligeuza na kurudi katika geti lake. Mamlaka yameanza kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo na kujua nia ya abiria huyo.
Mapema mwezi huu mamlaka ya anga ilifanya uchunguzi wa matukio mengi ya kukiukwa kwa sheria tangu mwaka 1995.
Matukio mengi yalihusishwa na abiria kukataa kuvaa barakoa. Wakala wa utafiti huo alisema abiria 394 waliingilia majukumu ya wafanyakazi wa ndege , iliripotiwa Mei 25.
Matukio haya ni mara mbili ya matukio yaliyotokea mwaka jana, ambapo kesi 183 zilifanyiwa uchunguzi.