Alikamwe "Mambo 10 nilioyaona Ruvu vs Yanga Leo"




1: What A Match🙌 WoW. Mpira mkubwa, mpira wa viwango.. Kwenye mbinu, kwenye Ufundi, Tumezipata Dakika 90 zilizojaa ubora mkubwa sana

2: Classic Goals🙌 Asante FeiToto! Asante Emmanuel Martin.. Asante Ntibazonkiza👏 Tutasifia ubora wa mbinu za walimu Lakini hatuwezi kusahau UFUNDI WA wanaume hao kwenye kuuweka mpira kambani

3: Kocha wa Yanga aliichukua mechi kwenye himaya yake katika dakika 45 za kwanza.. Feitoto akinufaika na mapafu ya Mukoko na akili ya Mauya kumtengenezea 'Pepo' mbele ya lango la Ruvu. Ni 'Utatu' huu ndio uliwapa Ruvu maswali mengi yasio na majibu

4: Kuumia kwa Mukoko kukaipa Mamlaka Ruvu kuuchukua mchezo kipindi cha pili. Yanga ilimkosa 'Box to Box' wa kuanzisha Pressing kwebye Mid block.. Ruvu wakaanza kuona nafasi na wakaenjoy mechi yao

5: Zawadi Mauya.. What A Player🙌 Hajafunga, Hajaasisti lakini ubongo wake ulipika mapishi mengi mazuri kwenye meza ya washambuliaji.. Alikuwa vyema kwenye kuusoma mchezo na kuvunja 'line za Ruvu' kwa pasi fupi fupi akiwa kwenye mwendo

6: Mukoko Tonombe🙌 INJINI ya Kikongo kwenye Gari ya Kijerumani. Mtu mkatili mwenye akili. Anakaba kwa kunusa hatari. Kifua chake kimejaa upepo wa kutosha. Ni 'Master' kwa kuhesabu hatua zake akifanya Pressing

7: Feisal Toto🙌 Bila shaka hii ni mecho yake bora msimu huu,👏 Alikuwa bora kwenye kujiweka kwenye maeneo sahihi na Ubora mkubwa katika Maamuzi yake.. WHAT A GOALS🙌 SO SPECIAL!

8: David Uromi.. 👍 Kasi yake, nguvu na uwezo wake wa kupiga pasi na kuingia katika maeneo uliwapa tabu sana mabeki wa Yanga muda ambao viungo wa Ruvu waliukamata mchezo

9: James Msuva alikuja 'kivulana' katika shughuli ya kiume. Kipindi cha pili Emanuel Martin alikuja kumuonyesha dhidi ya Yanga, Ruvu walihitaji akili, nguvu, kwenye kukaba na kushambulia ili kushinda mechi.. Mechi ilimkataa mapema sana.

10: Metacha Mnata! Kuna 'Ego' inaishi ndani yake. Ni kitu kibaya sana kwa career yake. Ni kama Mwili wake uko Yanga, akili imeshatoka. Anahitaji kufanya maamuzi ya haraka sana. Sina shaka na kipaji chake, ila kwa sasa anaonekana hayuko sawa kisaikolojia.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad