OFISA mzungu wa Polisi wa Minneapolis nchini Marekani ambaye alimuua kikatili na kinyama Mmarekani mwenye asili ya Afrika, George Floyd, Derek Chauvin ameiomba mahakama kumpunguzia hukumu au kumuweka chini ya uangalizi (probation) kufuatia waendesha mashtaka kumuomba Jaji atoe hukumu ya miaka 30 Jela.
Hukumu ya Derek Chauvin imetajwa kuwa itatolewa Juni 25, mwaka huu, kwenye maelezo yake, amesema sababu za kuomba kupunguziwa hukumu kutokana na kuhofia visa ambavyo vinaweza kumtokea kipindi akiwa jela.