Bila Barakoa Huingii Muhimbili

 


Dar es Salaam. Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imesema kuanzia kesho Jumatano Juni 23, 2021 itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuingia eneo la hospitali hiyo au kutoa huduma bila kuvaa barakoa na mgonjwa atatakiwa kuwa na msindikizaji mmoja tu.

Taarifa iliyotolewa leo Jumanne Juni 22, 2021 na mkuu wa kitengo cha mawasiliano kwa umma wa MNH,  Amaniel Aligaesha inaeleza kuwa hatua hizo zinatokana na maagizo ya waziri wa afya kwa taasisi mbalimbali akizitaka kuchukua tahadhari ili kujikinga na kuwakinga wananchi dhidi ya wimbi la tatu la ugonjwa wa Uviko-19 (Covid-19).

“Tunawaomba wananchi kuunga mkono hatua hizi ili kuongeza tahadhari ya kujikinga dhidi ya ugonjwa huu wa Covid-19. Utekelezaji wa maelekezo haya unaanza rasmi tarehe 23 Juni, 2021 (kesho).”

 “Tunawaelekeza wafanyakazi, wanafunzi, ndugu na jamaa wa wagonjwa wote wanaoingia eneo la hospitali kunawa mikono kwa kutumia sabuni na maji tiririka yaliyopo katika maeneo mbalimbali ya hospitali au vipukusi (sanitizer),” amesema.

Mbali na hayo MNH imeelekeza kwa wagonjwa waliolazwa wodini wataruhusiwa kuonwa na ndugu zao watano tu, asubuhi wataruhusiwa ndugu wawili, mchana ndugu mmoja na jioni ndugu wawili.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad