Msanii wa Nigeria Burna Boy leo Juni 10, 2021 amepokea tuzo (plaque) yake ya Grammy aliyoshinda Machi 16, 2020 katika msimu 63 wa tuzo hizo katika Kipengele cha Best Global Music Album kupitia album yake ya Twice As Tall.
Burna Boy ameposti picha na video mbalimbali za uthibitisho wa kupokea tuzo hiyo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii mapema leo na kuacha ujumbe unaoashiria ni kiasi gani ana furaha na kumshukuru Mungu.
Burna Boy ndiye mshindi wa kwanza wa Tuzo ya Afro-Beat kutoka Nigeria na amepokea tuzo yake hiyo ya Grammy huko Lagos, Nigeria.