Daktari wa Maradona akanusha kuhusika na kifo chake




Daktari wa magonjwa ya akili aliyekuwa akimtibu mcheza soka maarufu wa zamani wa Argentina Diego Maradona aliyefariki dunia Novemba mwaka uliopita amekanusha kuhusika kwa namna yoyote na kifo cha mchezaji huyo. 
Wakili wa daktari huyo amesema Agustina Cosachov ametoa ushahidi kwamba hakumuua Maradona baada ya kuitwa kwa mahojiano mbele ya ofisi ya mwendesha mashtaka ya mji wa San Isidro ulioko nje kidogo ya mji mkuu wa Argentina, Buenos Aires. 

Wakili wake amesema hakuna anayeweza kutuhumu kwamba dawa za matatizo ya akili ambazo daktari huyo alimpatia mteja wake zingeweza kusababisha moyo wa Maradona kushindwa kufanya kazi. 

Maelezo ya daktari huyo yanafuatia ripoti ya jopo la wataalamu iliyodai kwamba kulikuwa na uzembe uliopelekea kifo cha Maradona aliyeaga dunia akiwa na umri wa miaka 60 baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad