Shirika la Afya Ulimwenguni WHO, limesema nchi tajiri kiviwanda za kundi la G7 zina uwezo wa kutoa dozi milioni 100 za chanjo ya Corona kwa nchi maskini mwezi Juni na Julai pekee kusaidia kufikia malengo ya utoaji chanjo duniani kote katika mkutano wao wa kilele wiki hii.
FDA documents show Pfizer COVID vaccine protects after 1 dose | CIDRAP
Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amezihimiza nchi za G7 zizingatie usawa katika utoaji chanjo akisema kusaidiana chanjo ni muhimu kufikisha mwisho awamu ngumu ya janga la Corona.
Ghebreyesus amesema kufikia sasa asilimia 44 ya dozi zote zimetolewa katika nchi tajiri lakini asilimia 0.4 pekee zimetolewa katika mataifa maskini. Mkutano wa kilele wa matiafa ya G7 umepangwa kufanyika Cornwall, England, kuanzia Juni 11 hadi 13.