Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP), Sylvester Mwakitalu amemuondolea hati ya kuzuia dhamana aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (Rahco), Benhardard Tito.
Mbali na Tito, hati hiyo pia imeondolewa kwa wenzake wawili ambao ni mwanasheria wa zamani wa kampuni hiyo, Emmanuel Massawe na mwakilishi wa kampuni ya Rothschild (South Africa) Proprietary Limited, Kanji Mwinyijuma.
Watatu hao walikuwa wanakabiliwa na mashtaka nane likiwemo la kuisababishia Serikali hasara ya dola 527, 540 za Marekani sawa na Sh1.2 bilioni.
Dhamana ya washtakiwa hao ilizuiwa na DPP wa zamani, Biswalo Mganga kwa kuwasilisha hati ya kuzuia dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mwaka 2016.