Kirusi cha Delta kwa sasa ndicho kinachozungumziwa zaidi ulimwenguni, na wataalamu wengi wana wasiwasi juu ya kushika kasi kwa wimbi la tatu la maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya corona Covid 19.
Delta variant brings new pandemic threat to Germany | Germany| News and in-depth reporting from Berlin and beyond | DW | 17.06.2021
Kirusi cha Delta kiligunduliwa mwishoni mwa mwaka jana kilisababisha mlipuko mkubwa wa corona mwanzoni mwa mwaka huu nchini India. Sasa nchi hiyo imebaini kirusi kipya ambacho kinatokana na Delta ambacho kimepewa jina la Delta Plus.
Kirusi hicho kipya “kimeitia nchi hiyo wasiwasi,” ingawa kulingana na wataalamu inawezekana kuwa bado ni mapema mno kuanza kuwa na uwoga.
Mabadiliko ya kirusi hicho ambacho kilikuwa “kinachofuatiliwa” na kuwa “kinachotia wasiwasi” kutokana na ushahidi kwamba kinafikia moja ya vigezo kadhaa: kinaweza kusambaa kwa haraka, kinasababisha hali ya mgonjwa kuwa mbaya zaidi, kupunguza ufanisi wa dawa na chanjo na kadhalika.
Wizara ya Afya nchini India imesema kuwa tafiti kadhaa zimeonesha kwamba kirusi cha delta plus ambacho pia kinafahamika kama AY.1, kinasambaa kwa haraka sana, kina athiri mapafu kwa urahisi na pia ni vigumu kutibika kwa dawa zilizopo.
Wizara ya Afya imesema kuwa kirusi delta plus mara ya kwanza kilibainika nchini humo mnamo mwezi Aprili kwa karibu watu 40 kutoka maeneo sita katika majimbo matatu ya Maharashtra, Kerala na Madhya Pradesh.
Takriban vipimo 16 vya virusi hivyo vilibainika huko Maharashtra, moja ya majimbo yaliyoathirika vibaya na janga la virusi vya corona.
Kirusi cha delta plus pia kimebainika katika nchi 9 (Marekani, Uingereza, Ureno, Switzerland, Japani, Poland, Nepal, Urusi na China). Kirusi cha awali chaDelta kimeshathibitishwa kusambaa katika nchi 80.
Ukosefu wa data
Coronavirus
Mamia ya maelfu ya chembe za vinasaba vinatathminiwa kote duniani.
Virusi hubadilika kila wakati lakini mabadiliko mengine hufanya magonjwa kuwa ya kuambukiza zaidi au hata kuwa tishio na mabadiliko haya huonekana kukithiri.
Na hasa katika hili, mtaalamu wa magonjwa ya virusi amehoji ikiwa kimebainishwa kama chenye kutia wasiwasi,” na kusema kuwa bado hakuna data inayothibitisha kwamba kirusi hicho kina ambukiza zaidi au kinafanya mtu kuwa mgonjwa zaidi kikilinganishwa na virusi vingine.
“Bado hakuna taarifa zozote kuunga mkono madai ya kwamba kirusi hiki ni chenye kutia wasiwasi,” amesema Gagandeep Kang, mtaalam wa magonjwa ya virusi na mwanamke wa kwanza kutoka India kuchaguliwa katika taasisi ya wataalamu ya Kifalme ya London.
“Unahitaji taarifa za kibaolojia na za hospitali kufikia hitimisho kama kweli ni kirusi kibaya na kwa kiasi gani.”Reino Unido
Virusi vya Delta na Delta Plus vimethibitishwa kuingia Uingereza.
“Unahitajika kufanya utafiti kwa mamia ya wagonjwa wenye hali kutokana na kirusi hichi na kubaini ikiwa wako katika hatari ya kuwa wagonja zaidi ikilinganishwa na virusi vilivyotangulia,” Kang amesema.
Faida kidogo
Kirusi cha delta plus kina mabadiliko mengine yale yanayofahamika kama K417N katika protini ya virusi vya corona, ambayo imepatikana kwa virusi vya beta na Gamma, mara ya kwanza kubainika ni Afrika Kusini na Brazil mtawalia.
Hata kwa vipimo 166 vya virusi vya delta, “hatuna sababu kubwa ya kutufanya tuamini kwamba ni hatari zaidi kuliko kirusi cha delta halisi.”
“Pia kirusi cha delta plus kina mabadiliko kidogo katika maambukizi na kusambaa miongoni mwa watu wengine ambao awali waliwahi kuwa na maambukizi wenye kinga dhaifu au ambayo haijakamilika inayotokana na chanjo,” Kamil ameiambia BBC.India
Ni jambo la kawaida tu
Anurag Agarwal, mkurugenzi wa taasisi ya chembe za urithi huko New Delhi, moja ya maabara 28 nchini India ilisema kuwa “familia yote ya virusi vya delta ni vyenye kutia wasiwasi”, kwahiyo, hakukuwa na ubaya wowote kubaini kirusi cha delta plus kuwa miongoni mwa kundi hilo.
“Hatuna kinachoonesha kuwa kirusi cha delta plus kinastahili kusababisha wasiwasi au taharuki katika afya ya umma. Tunakifuatilia kwa makini na kuimarisha hatua zote za afya,” amesema.
Kamil ameongeza kuwa serikali ya India “ingechukua hatua sasa hivi badala ya kusibiri kama ilivyokuwa kwa kirusi delta.”
Na wanasayansi wengi wamekiri kuwa kushindwa kuchukua hatua stahiki kama majaribio ya kutosha ya kirusi hicho ambacho kilisababisha wimbi la pili la virusi vya corona nchini India mnamo mwezi Aprili na Mei kunaweza kuwa na athari kubwa.
“Sio kwamba nina wasiwasi sana. Lakini ni sawa kufuatilia kirusi hicho kwa karibu mno.”