Fahamu Kuhusu Jamii ya Illuminati



Jamii hiyo ilizua nadharia kwa miaka mingi , huku watu wakidai kwamba ni shirika moja la kisiri ambalo nia yake ni kuteka uuongozi wa dunia.

Mbali na kuwa chanzo cha mapinduzi makubwa duniani na mauaji. Lakini Illimunati ni akina nani na je ni kweli walidhibiti ulimwengu?

1. Je ni akina nani walioanzisha Illuminati

Jamii ya iluminati ilikuwa jamii ya siri iliobuniwa nchini Bavaria kwa sasa Ujerumani ambapo ilikuwepo kuanzia 1776 hadi 1785 ambapo wanachama wake walikuwa wakijiita wakamilifu.

Kundi hilo lilianzishwa na Profesa wa sheria Adam Weishaupt. Alitaka kukuza elimu ya fikra ili kupinga uchawi na ushawishi wa kidni katika jamii.

Weishaupt alitaka kubadilisha jinsi serikali zilivyoendeshwa barani ulaya , akiondoa ushawishi wa kidini katika serikali na kuwapatia walimwengu muongozo mpya .

Inaaminika kwamba mkutano wa kwanza wa iluminati huko Bavarian ulifanyika katika msitu karibu na Ingolstadt mwezi Mei tarehe mosi 1776.

Wakati huo, watu watano walianzisha sheria ambazo zingetawala siri ya utawala wa Iluminati.

Kwa muda sasa, lengo la kundi hilo liliangazia kuhusu kushawishi maamuzi ya kisiasa na kumaliza taasisi kama zile za kifalme na kanisa.

Baadhi ya wanachama wa Iluminati walijiunga na kundi la Freemasons ili kusajili wanachama wapya.

Ndege mmoja anayejulikana kama Minerva Owl alitumika kuwa nembo yake.

Ndege huyo alikuwa mnyama mtakatifu wa mungu wa kike Athens katika hadithi za Uigiriki, na katika tamaduni za Kirumi, ndege wa Minerva.

2.Je iluminati wanahusiana vipi na Freemasons?

Masoni ni agizo la kindugu ambalo lilikua kutoka kwa vikundi vya waashi wa mawe na wajenzi wa kanisa kuu la zama za Kati.

Katika nchi zingine, haswa Marekani, kihistoria kumekuwa na hisia fulani kuhusu Freemason; Mnamo 1828, harakati moja ya kisiasa inayojulikana kama Chama cha Kupambana na Mason ilianzishwa .

Kwa sababu awali Illuminati iliwasajili Freemason, vikundi hivyo viwili mara nyingi vilishukiwa kuwa na uhusiano.

3.Je unawezaje kujiunga na illuminati?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad