Bila shaka umesikia simulizi nyingi za kuvutia kuhusu milki nyingi hadi kufikia hii leo. Ikiwa ni pamoja na Milki ya Uingereza, utawala wa Genghis Khan kutoka China hadi India au Milki ya Mughal kutoka Kabul-Kandahar hadi Karnataka.
Lakini leo hii tunakufahamisha kuhusu moja ya milki ndogo zaidi duniani. Cha ajabu ni kwamba, ni watu 11 wanaishi katika eneo hili.
Katika milki hii kuna mfalme anayesimamia boti na kuendesha mgahawa wa pekee yeye mwenyewe. Eneo hili la Kifalme lenye kuvutia linajulikana kwa jina Falme ya Tavolara.
Kisiwa kidogo
Ni kisiwa kidogo katika bahari ya Mediterranean karibu na Sardinia huko Italia. Eneo hilo la kifalme limekuwepo kabla Italia haijatambuliwa kama nchi.
Ufalme wa Tavolara upo katika kisiwa kidogo cha Tavolara. Eneo hilo lina ukubwa wa kilomita 5 za mraba.
Mfalme wa eneo hili anaitwa Antonio Bartalioni lakini utakapotembelea eneo hili unaweza kuwa na wakati mgumu kumtambua kwasababu mwenyewe haonekani kama mfalme. Yaani hakuna kitu kama mavazi au mtindo maalum wa maisha. Antonio Bertaloni anasema kuwa kama mfalme, anachopata yeye ni chakula cha bure pekee kutoka kwa mgahawa wake.
Nchi zingine ndogo kama Tavolara
1. Redonda - Eneo hili la Southampton huko England lilijitangazia uhuru wake kukwepa marufuku ya kutovuta sigara.
2. Tavolara - eneo hili lina ukubwa wa kilomita 5 za mraba nchi yenye jumla ya watu 11 pekee. Mfalme Antonio anaendesha mgahawa pekee eneo hili.
3. Tonga - nchi hii ipo katika bahari ya Pasifiki eneo la kilomita 748 za mraba. Eneo hili liligunduliwa mwaka 1773 na nahodha James Cook. Nahodha Cook akalipatia jina 'Kisiwa cha Urafiki' lakini ukweli ni kwamba wenyeji walitaka kumuua nahodha Cook.
4. Brunei - ni eneo lenye ukubwa wa kilomita 5,765 za mraba, Brunei ina idadi ya watu 4,13,000. Watu hapa hawahitajiki kulipa kodi. Sultan wa Brunei ni mmoja kati ya watu matajiri zaidi duniani.
5. Swaziland - Hii ni nchi iliyopo Afrika na ukubwa wake ni 17, 363 kilomita za mraba. Kwasababu ya asili ya eneo hilo zuri, linaitwa nchini ya maajabu.
6. Lesotho - Ipo Afrika Kusini. Nchi hii ina ukubwa wa kilomita 30,000 za mraba. Katika maeneo ya chini idadi ya watu ni takriba n milioni 2.
Mfalme Dame wa Tavolara
Mfalme wa Tavolara anasherehekea maadhimisho ya miaka 180 mwaka huu.
Na watu wa eneo hili pamoja na Mfalme Antonio Bartalioni wanalichukuliwa kwa uzito mkubwa. Alipoulizwa kuhusu maadhimisho hayo, alielezea historia ya vizazi vingi vilivyopita.
Kulingana na Antonio Bertalioni, baba mkwe wake, Giuseppe Bartalioni, alikimbilia Italia mwaka 1807 baada ya kuoa dada wawili. Wakati huo, Italia haikuwa nchi lakini Sardinia ilikuwa sehemu ya Italia ikijiendesha kama milki. Ilikuwa uhalifu kuoa wake wawili katika eneo hili. Kwa hiyo Giuseppe Bartalioni akakimbilia kisiwani na kuanza maisha mapya huko.
Ufugaji wa mbuzi
Giuseppe alikuwa anatoka mji wa Geneva. Na ndani ya siku kadhaa wakajifunza kuhusu ufugaji wa mbuzi katika kisiwa hicho.
Aina ya mbuzi aliyekuwa anapatikana huko alikuwa pekee wa aina hiyo duniani.
Na ndani ya siku chache tu, taarifa za mbuzi hao zikawa zimefika Italia. Mfalme Carlo Alberto wa Sardinia akafika katika kisiwa cha Tavolara kujionea na kuanza kutafuta wake.
Mwaka 1836, Giuseppe, kijana wa Paolo alimsaidia Carlo Alberto kutafuta mbuzi na kuzunguka eneo lote la kisiwa hicho. Antonio anasema Mfalme Alberto wa Sardinia alipowasili kisiwani humo, alijitambulisha. Wakati huo, Paolo naye akijitambulisha kama Mfalme wa Tavolara.
Bahari ya Mediterranean
Carlo Alberto aliporejea nchini mwake baada ya ziara yake ya siku tatu huko Tavolara, alitoa agizo akitangaza kuwa Tavolara kuwa sio sehemu ya jimbo la Sardinia. Paolo Bartalioni naye akajitangaza kuwa mfalme. Wakati huo kulikuwa na jumla ya raia 33 pekee kisiwani humo. Kwahiyo, Paolo akawa Mfalme wa watu hao 33.
Paolo alijenga kaburi lake la kifalme kabla ya kufariki dunia. Aliandika katika wasio wake kwamba taji liwekwe kwenye kaburi lake baada ya kifo chake.
Cha ajabu ni kwamba yeye mwenye hakuwahi kuvaa taji wakati akiwa hai.
Mkataba wa amani
Wafalme wa Tavolara pia nao walifikia makubalino nan chi nyigi tu. Ilijumuisha Garibaldi, inayotambulika kama mwanzilishi wa Italia.
Kisha Mfalme wa Sardinia, Vittorio Emmanuel II, akatia saini mkataba wa amani na Tavolara mwaka 1903
Uwepo wa wanajeshi wa NATO
Kujitawala kwa eneo hili dogo la kifalme kulifikia mwisho pale wanajeshi wa Nato walipoamua kuweka kambi yao eneo hilo.
Hakuna aliyeruhusiwa kuingia wala kutoka. Lakini Italia haijawahi kukubali au kuchukua Tavolara kama sehemu yake.
Pia hakuna nchi ambayo imetambua eneo la Tavolara. Mfalme Antonio Tavalara na familia yake wanaendesha boti la abiria ambalo husafirisha watalii kutoka Italia hadi katika kisiwa ivho.
Huwa wanatembelea eneo hili kujionea spishi ya mbuzi ambayo ipo hatarini kupotea kabisa na mwewe.