Fahamu Utabiri na utata uliomzunguka TB Joshua





Licha ya kuwa na wafuasi chungu nzima kutoka mataifa tofauti duniani, pia alikuwa na wakosiaji wengi vilevile kutokana na mafunzo ya kanisa lake.


Hii leo tunakuangazia kuhusu utabiri aliotoa na utata uliomzunguka.



Maji ya Upako

Mwaka 2013 hamu ya maji ya upako{ Maji matakatifu} ya TB Joshua yalizua mkanyagano uliosababisha vifo vya watu wanne katika kanisa moja lililopo katika mji mkuu wa Ghana Accra.



Maelfu ya watu waliokimbilia maji hayo 'matakatifu waliamini kwamba yana uwezo wa kutibu.



Chombo cha habari cha AFP kiliripoti kwamba mkanyagano huo ulitokea wakati waumini walipoanza kusukumana kwenda kupata maji hayo mbele ya kanisa hilo.



Wengi walimkosoa TB Joshua baada ya tukio hilo lakini maafisa wa polisi nchini Ghana wanasema ni vigumu kutupia mtu lawama.



Msemaji wa polisi Freeman Tetteh wakati huo aliesma kwamba watachunguza kubaini ni nani wa kulaumiwa.



Mwaka 2014, paa la nyumba moja ya wageni iliopo ndani ya kanisa la SCOAN la muhubiri huyo katika eneo la Ikotun -Egbe mjini Lagos lilianguka .



Idadi ya watu waliofariki kutokana na kuanguka kwa jumba hilo ilifikia 115, ikiwemo raia 84 wa Afrika Kusini kulingana na waziri mmoja wa taifa hilo, Jeff Radebe.



TB Joshua alilaumiwa kuwa chanzo cha kuanguka kwa jumba hilo.



Alidai kwamba baadhi ya watu walitaka kumuua kupitia tukio hilo.



Wakati huo, rais wa Nigeria Goodluck Jonathan alitembelea kanisa hilo na kuamua kuanzisha uchunguzi kuhusu kile kilichotokea.



'Miujiza yenye utata'



Lakini mzozo uliokuwa ukimzunguka muhubiri huyo haukuishia hapo, kwasababu wengi pia walimkosoa kuhusu miujiza yake mingi katika mikutano yake.



Mwaka 2017, Chris Okotie, muhubiri Maarufu nchini Nigeria , alimshutumu Joshua kwa kufanya 'uganga'.



Lakini waziri wa zamani wa usafari wa ndege , Femi Fan Kayode ambaye alikuwa rafiki wa karibu wa TB Joshua alimtaka Okotie kuwacha kumshambulia Joshua na badala yake kuitisha umoja katika kanisa hilo.



Wakosoaji wake wa Kikristo wamekuwa wakisema kwamba mbinu anazotumia TB Joshua haziendani na zile zilizopo katika bíblia.



Baraza la Kanisa la Pentecostal nchini Nigeria halikukubali kanisa la Joshua kuwa chini yake.



Youtube yampiga marufuku TB Joshua



Mwaka 2021, mtandao wa Youtube uliondoa runinga yake ya Emmanuel TV katika mtandao huo kutokana na matamshi ya chuki baada ya kanda moja ya vídeo ya muhubiri huyo akijaribu kutoa mapepo katika miili ya wapenzi wa jinsia moja kuzua hisia kali.



Baadaye mtandao wa Facebook uliondoa kanda zote za vídeo za ibada hiyo.



Ebola Afrika Magharibi

Wakati mlipuko wa Ebola ulipozuka Afrika ya magharibi , serikali ya jimbo la Lagos iligundua jinsi idadi ya watu ilivyoongezeka katika kanisa la TB Joshua, ikilazimika kuwaomba raia kutowapeleka wagonjwa wa maradhi hayo katika kanisa hilo ili kuzuia usambazaji wa ugonjwa huo.



TB Joshua alikubali kusimamisha baadhi ya mipango ya kutibu ya kanisa hilo lakini akatuma chupa 4,000 za maji ya upako nchini Sierra ili kutibu ugonjwa huo.



Utabiri wa TB Joshua

Muhubiri TB Joshua kama alivyo maarufu kwa utabiri anadaiwa kubashiri kifo cha Michael Jackson, Kupotea kwa ndege ya Malaysia MH370 na nyenginezo.



1.Michael Jackson



Kuhusu kifo cha Michael Jackson, Aliwaambia waumini wake kwamba ''umaarufu wangu ni mkubwa kwasababu watu wanajua niko kila mahali''.



''Naona kutatokea kitu kikubwa kwa nyota huyo ambaye ataondoka na kwenda mahali ambapo hatorudi tena na najua siku atakayokwenda''



Na baada ya kifo cha Michael Jackson , TB Joshua alisema kwamba huo ulikuwa utabiri alioutoa miezi sita iliopita.



Lakini watu wamekuwa wakikosoa mafunzo yake ya utabiri na kudai kwamba amekuwa akitumia fursa za matukio kujipigia debe.



2. Virusi vya Corona

Mwaka uliopita , wakati mlipuko wa corona ulipoanza , TB Joshua alisema kwamba virusi vya ugonjwa huo vitaisha mwezi Machi wakati wa ibada moja lakini baada ya virusi hivyo kuendelea kuuwa watu, alienda mlimani kufanya maombi ili virusi hivyo viondoke.



Lakini licha ya utata unaomzunguka , waumini wamekuwa wakijaa katika kanisa lake ili kuomba mwongozo.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad