Gigy Money aachiwa huru




Msanii wa Bongo Fleva, Gigy Money amesema sasa yupo huru baada ya kumaliza adhabu yake aliyopewa na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) ya kutojihusisha na sanaa ndani na nje ya nchi kwa kukiuka maadili ya kazi za sanaa.
Gigy amethibitisha hilo kupitia instagram yake kwa kuandika ‘’tumefunguliwa’’ baada ya BASATA Januari 5, mwaka huu kupitia kwa Kaimu Katibu Mtendaji wa baraza, Matiko Mniko,kutangaza kumfungia kutojihusisha na shughuli za Sanaa baada ya msanii Gigy kutumbuiza jukwaani akiwa amevalia nguo zilizodhalilisha utu wake na kubugudhi hadhira ya wapenda sanaa.
Tukio hilo lilitokea akiwa katika tamasha la muziki huko jijini Dodoma katika uwanja wa Jamhuri.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad