Harmonize amedokeza ujio wa kazi mpya kutoka kwenye album yake ya pili 'High School' ambayo anatarajia kuachia mwaka huu.
Kupitia insta-story yake ameonesha kujigamba kuwarejesha Club watu kupitia ujio wake huo mpya ambao mpaka sasa hajaweka wazi ni lini ataachia mradi huo.
“Kondeboy take them back to the club”, “Smash hit way 2 the album dem deady”
Bosi huyo wa lebo ya Konde Music Worldwide (KMW) kwa muda sasa amekuwa busy akitayarisha album hiyo ambayo amewashirikisha wasanii mbalimbali ikiwa ni pamoja na mwanadada Busiswa Gqulu kutokea Afrika Kusini