Hatima ya Seth na Rugemarila Yamsubiri DPP




Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, mazungumzo ya makubaliano (Plea bargain) ya kumaliza kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mkurugenzi wa Kampuni ya Kufua Umeme (IPTL), Herbinder Seth yanasuburi Muongozo wa Mkurugenzi mpya wa Mashtaka (DPP).

 

Wakili wa serikali Mwandamizi Wankyo Simon ameeleza hayo leo Juni 3, 2021 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa na kujua hatma ya mazungumzo hayo na upelelezi ulipofikia.

 

“Mheshimwa Hakimu, kesi imekuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado, mazunguzo ya kumaliza kesi dhidi ya mshtakiwa Seth yanaendelea pale yalipoishia, tunasuburi muongozo kutoka kwa Mkurugenzi wa mashtaka DPP mpya aliyeteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ili tuweze kuwakilisha hapa mahakamani.

 

Awali Seth na Makandege waliwasilisha ombi kwa DPP wakionesha nia yao ya kutaka kumaliza kesi kwa kukiri makosa yao lakini, Mei 6, 2021 Wakili Makandege aliondoa nia yake ya kufanya makubaliano na DPP akieleza kwamba mazungumzo hayo hayana afya na yamechukua muda mrefu kukamilika.

 

Mbali na Seth washtakiwa wengine Katika kesi hiyo ni mfanyabiashara James Rugemalira na wakili Joseph Makandege.

 

Rugemarila, ambaye ni Mkurugenzi wa VIP na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL na Seth ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa PAP, wanadaiwa kutenda makosa hayo katika Jiji la Dar es Salaam na nchi za Afrika Kusini, Kenya na India.

 

Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka 12 yakiwemo ya utakatishaji fedha, miongoni mwa mashtaka hayo yapo ya kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu, kughushi na kutoa nyaraka za kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kutakatisha fedha na kusababisha hasara ya Dola za Marekani 22,198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad