Hatimaye Mahakama Kuu yamrejeshea Fatma Karume uwakili




MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imefuta uamuzi wa Kamati ya Maadili ya Mawakili Tanganyika, wa kumfuta uwakili, Mwanaharakati Fatma Karume. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Kamati hiyo ilimvua uwakili Fatma na kuondoa namba yake ya uwakili ( 848), katika orodha ya mawakili wa Tanganyika, tarehe 23 Oktoba 2020, kwa tuhuma za kukiuka maadili ya taaluma hiyo, katika kesi ya kupinga uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Prof. Adelardius Kilangi.

Kwa mujibu wa Wakili wa Fatma Karume, katika Kesi ya Rufaa Na. 2/2020, iliyofunguliwa Mahakama Kuu kupinga uamuzi huo, Rugemeleza Nshala, mwanaharakati huyo amerudishiwa uwakili wake.

Dk. Nshala amesema kuwa, uamuzi uliotolewa na jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo, leo tarehe 21 Juni 2021, umeamuru sakata hilo lirudiwe kusikilizwa upya katika kamati hiyo, ili kumpa Fatma nafasi ya kujitetea.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad